Shughuli Zetu

SHIRECU inajishughulisha na kazi zifuatazo, kwa mujibu wa masharti ya Sheria yake:-

  1. Kununua pamba kutoka kwa wakulima kupitia vyama vyao vya msingi, chini ya masharti na sera zao huria.

  2. Kusafirisha/kusafisha mbegu za pamba, nyuzinyuzi za pamba, mbegu za pamba na mazao mengine ya ziada ya pamba na pembejeo za kilimo kwa kutumia magari yake, hadi maeneo mbalimbali kama inavyotakiwa.

  3. Kusimamia na kuendesha viwanda vyake 2 vya kuchambua pamba (ginneries) na kiwanda kingine 1 cha kusindika mafuta ya pamba (oilmills).

  4. Kusambaza elimu ya ushirika kwa wakulima, vyama vya ushirika wanachama, bodi za ushirika na wafanyakazi wao.

  5. Kununua na kuuza pembejeo kwa wakulima kupitia vyama vyao vya msingi vya ushirika.

  6. Kuhimiza wakulima kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika.

  7. Kusambaza elimu ya kilimo na ubora wa mazao kwa wanachama wake kwa njia mbalimbali.