UMUHIMU

UMUHIMU WA USHIRIKIANO KATIKA MKOA WA SHINYANGA

Vyama vya Ushirika ndiyo silaha pekee iliyobaki na ya uhakika ya kumuinua mkulima wa kipato cha chini, kupitia Vyama vya Ushirika Wakulima wana sauti moja katika kuamua mambo kama kupanga bei ya mazao yao wanapotaka kuuza, kutafuta soko la uhakika, ikiwa ni pamoja na kuzalisha kwa tija. Aidha, kupitia Vyama vya Ushirika wakulima kwa kiasi kikubwa wanapata faida kubwa kwa sababu wao ndio wanaopanga bei, mfano mzuri ni kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

  • Kupitia mtindo wa ushirika kwa mkoa wa Shinyanga, wakulima watanufaika kwa kiasi kikubwa kwani licha ya kuwa na zao la pamba kwa muda sasa, Serikali imehalalisha rasmi uuzaji wa zao la Dengu na Choroko kwa njia ya minada, hivyo kuwaongezea kipato wakulima wadogo.

 

  • Kuongezeka kwa uelewa na umuhimu wa wakulima kutumia vyama vya ushirika ili kupata tija na kuepuka wizi au hasara. Kwa mfano, kwa mwaka 2020/2021, SHIRECU (1984) LTD imepanga kutumia mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa wakulima kuuza mazao yao, mfumo ambao kimsingi ni agizo la Serikali yetu pendwa ya Awamu ya Tano.