Historia ya SHIRECU

Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) LTD kilisajiliwa Aprili 4, 1984 na kupatiwa Cheti cha Usajili Namba 4123. Hata hivyo kwa mujibu wa mabadiliko ya Mfumo wa Uendeshaji wa Vyama vya Ushirika (MUVU) mwaka 2022, Chama kilifanikiwa kupata usajili mpya wenye namba AFF-MCY20-20SH. Hivi sasa, SHIRECU (1984) LTD inaundwa na Vyama vya Msingi 107 ambavyo vinajishughulisha zaidi na pamba na mazao mengine mchanganyiko kwa maana ya Dengu na Choroko. Aidha, Chama kina jumla ya wanachama zaidi ya 38,178 wanaounda Vyama 107 vya Msingi.