MAONESHO YA 32 YA WAKULIMA (NANENANE) LEO KATIKA VIWANJA VYA NZUGUNI JIJINI DODOMA.
Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) LTD Kimeshiriki maonyesho ya 32 ya wakulima nanenane katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
Watu mbalimbali wameweza kujifunze fursa mbalimbali za maendeleo kupitia ushirika, kilimo Cha zao la Pamba, Alizeti, Dengu na Choroko pamoja na namna bora ya Uendeshaji wa SHUGHULI za Chama kikuu Cha ushirika SHIRECU kinavyojikita kwenye kilimo bora na chakisasa Cha mazao mchanganyiko na kutoa elimu kwa Wakulima/wanachama pamoja na kuwatafutia masoko ya uhakika.
Maonyesho hayo yanaendelea hadi siku ya kilele katika Banda la Ushirika la Mkoa wa Shinyanga katika kijiji cha Ushirika.
Aidha, Chama kikuu cha Ushirika SHIRECU kinawakaribisha watanzania wote kuja kujionea fursa za uwekezaji na huduma mbalimbali ikiwa ni Pamoja na:-
i. Uwekezaji katika viwanda vya kuchakata pamba.
ii. Kilimo cha mazao mchanganyiko choroko, dengu, alizeti, mpunga na fursa ya kilimo cha zao la pamba.
iii. Fursa ya elimu ya kilimo bora na masoko ya mazao.
iv. Upangishaji wa maghala yaliyoko Bandari ya Dar es salaam Pamoja na mkoa wa Shinyanga
v. Upangishaji wa nyumba za kuishi pamoja na ofisi, zilizoko Dar es salaam pamoja na mkoa wa Shinyanga
vi. Fursa ya elimu kupitia shule yetu ya sekondari ya Buluba iliyoko mjini shinyanga.
vii. Fursa ya mikopo ya uwezeshaji kwa vyama wanachama na kupitia saccos ya chama kikuu cha Shirecu (1984) limited.
viii. Upatikanaji wa pembejeo bora, ikiwemo mbegu bora, viuatilifu, zana mbalimbali za kilimo kupitia duka letu la ushirika Shirecu lililopo mjini shinyanga.